Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe waondoa hofu wateja ubora wa parachichi

Bashe Kilimo Bajeti Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema parachichi za Tanzania zimekithi vigezo vya kimataifa na ndio maana Tanzania imekuwa nchi pekee ambayo imeruhusiwa kuingiza bidhaa hiyo katika soko la India.

Bashe ameyasema hayo jana Jumanne Mei 31, 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini (CCM), Deodatus Mwanyika.

Mbunge huyo alitaka kufahamu Serikali ina kauli gani kuhusu taarifa za hivi karibuni mtaani zinazosema parachichi ya Tanzania sio bora.

Akijibu swali hilo, Bashe amesema parachichi ya Tanzania inapotoka nje ya mipaka ina vyeti vyote vya kimataifa vya viwango.

“Ndio maana tumekuwa tukifungua masoko mapya na hivi karibuni tumefungua soko la India na Tanzania pekee ndio imeruhusiwa kuingiza parachichi soko la India.”

Amewataka wasafirishaji wa Tanzania kuweka nembo ya biashara kuwa bidhaa hiyo imezalishwa nchini.

Advertisement “Ushindani upo watu watataka kuharibu taswira yetu na yeyote mwenye mashaka awasiliane na Wizara ya Kilimo na sisi tupo tayari kulinda bidhaa yetu popote pale,”amesema Bashe.

Katika swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ritta Kabati ametaka kujua nini mkakati wa Serikali kuondoa vikwazo kwa magari makubwa ambayo yanasafirisha parachichi kwenda nchi za nje kwa kuoga vibali kwa saa 24 badala ya saa 12.

Akijibu swali hilo, Bashe amewataka wakulima wa parachichi mkoani Iringa wazalishe parachichi kwa tija.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itaendelea kuhamasisha wadau kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi kutoka tani 190,000 mwaka 2018 hadi kufikia tani 215,000 mwaka 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live