Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe azicharukia kampuni za kuuza mbegu... aapa kuzifuta!

Bashe3 Bashe azicharukia kampuni za kuuza mbegu... aapa kuzifuta

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hatosita kuzifutia leseni kampuni za mbegu ikiwa zitakiuka makubaliano waliyoyafikia na Serikali juu ya bei za mbegu.

Bashe amesema kampuni hizo zimepatiwa ardhi ya Serikali ili wazalishe mbegu na makubaliano ya mbegu elekezi yamefanyika kwa bei za jumla na rejareja hivyo kufikia tarehe 20 bei elekezi ya mbegu za mahindi itatangazwa kwenye magazeti kwa nchi nzima.

Akizungumza wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Manyara, Bashe amesema makubaliano yamefanyika na kampuni ya Seedco kuwa bei iwe kati ya 12,000 hadi 14,000 hivyo hatosita kuzifutia leseni za kuuza mbegu hapa nchini ikiwa watayakaidi maakubaliano hayo.

“Na wanielewe kabisa nasema mbele ya mwenye nchi Rais wetu, sitasita kuwafutia leseni ya kuuza mbegu katika nchi wakienda kinyume na maelekezo na makubaliano tuliyokubaliana. Wameomba ardhi kwenye mashamba ya Serikali tumewapa mashamba tunawawekea miundombinu ya uzalishaji na umwagiliaji ili waweze kuzalisha mbegu wauze kwa bei tunazokubaliana.

Na wewe Agro dealer ambaye tumekupa leseni na bahati mbaya unaweza ukawa na leseni ya biashara mimi nikakufutia leseni ya kuuza mbegu, inakula kwako ukienda kinyume na bei tunazotangaza kuanzia tarehe 20 za bei elekezi za mbegu,” amesema Bashe.

Amesisitiza kuwa ameielekeza kampuni ya mbegu Seedco kutoa matangazo ya bei za mbegu zao kupitia magazeti kama yalivyokuwa makubaliano ili bei hiyo ujulikane.

Aidha, amewataka wakuu wa wilaya baada ya kupatiwa waraka kutoka Serikalini, kutembelea maduka yote ya mbegu ili kuwabaini wanaouza mbegu nje ya bei rasmi waliyokubaliana Serikali na kampuni za mbegu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live