Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe atoa maelekezo soko la sukari

73579898a2178cb674c148cdef0ce8ba Bashe atoa maelekezo soko la sukari

Fri, 15 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe, amewataka wadau wa sukari kuwa na imani na kujenga uhusiano mzuri na Bodi ya Sukari, ili kuimarisha zao la miwa na kukuza soko la sukari nchini.

Bashe ameyasema hayo leo mchana Julai 15, 2022, kwenye ukumbi wa hotel ya Morogoro, wakati akizindua Kongamano la 10 la wadau wa sukari, ambapo lilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji.

Waziri Bashe amesema Serikali ya Awamu ya Sita, imesikia hofu waliyonayo wadau sukari juu ya sera na kuwahakikishia kuwa serikali italinda uwekezaji wao wanaofanya nchini pamoja na kuwaunga mkono katika juhudi zao za uzalishaji wa sukari.

Ameiagiza Bodi ya Sukari pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), kuanzisha mashamba ya kuzalisha mbegu bora, ili kuongeza tija na uzalishaji zaidi wa miwa nchini.

“Tuna aina mbili za mbegu ya zao la miwa, ni lazima tukubaliane kuanzisha mashamba yatakayozalisha mbegu,” amesisitiza Waziri Bashe.

Waziri Bashe pia ameagiza kufanyiwa maboresho kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Sukari, ili uweze kutatua changamoto mbalimbali na kuendeleza tasnia hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live