Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe atangaza neema kwenye kilimo

Bashepiic Data Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujayo.

Bashe ameomba fedha hizo leo Jumatatu Aprili 4, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.

Bashe amesema bei ya mbolea katika soko la dunia imepanda kwa zaidi asilimia 300.

Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.

Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais fedha hii haitapotea. Tumeshafanya hivi katika korosho kwa kugawa ruzuku ya pembeje na tumeongeza uzalishaji tani 40,000,”amesema.

Advertisement Aidha, Bashe amesema  jumla ya maofisa ugani 7,000 watagawiwa pikipiki na vifaa vya kupimia udongo.

“Tumeanza kuwapa elimu maofisa ugani kulingana ekolojia ya maeneo na mazao yanayozalishwa na tutawapa ekari moja kwa  kila ofisa ugani, atapewa mbegu bora na mbolea ili akiwafundisha awapeleke shambani,”amesema.

Amesema kuwa majaribio yameanza katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kwa kutenga mashamba 600 ambapo kila kijiji kitakuwa na shamba darasa ili wakulima wapate elimu stahiki.

Pia amesema maofisa ugani hao watapatiwa vifaa vya kupimia udongo na kwamba hapo mwanzo taarifa za udongo zilikuwa zinapatikana kama za uganga wa kienyeji.

Bashe amesema lengo hadi kufikia mwaka 2025 kila kata iwe na kipimia udongo chake ambapo mkulima atapimiwa udongo na kupewa cheti ambacho kitakuwa na taarifa zote za afya ya udongo wake na aina ya virutubisho vinavyotakiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live