Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe ataka wakulima wauze mazao bila kuzuiwa

69730 PIC+BASHE

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Naibu waziri wa Kilimo nchini Tanzania,  Hussein Bashe amewataka wakuu wa Wilaya nchini kutowadhibiti wakulima kuuza mazao yao.

Bashe ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 3, 2019 wakati akifungua maonesho ya Nanenane  Mikoa ya Kagera,  Geita na Mwanza yaliyofanyika viwanja vya Nyamhongoro jijini Mwanza.

"Nataka niwaulize hata kama tumejaza mahindi hiki kiwanja chote kama hamna hela ya kuyanunua hayo mahindi yatawasaidia? Wakulima wanalima mazao ya kilimo, ya chakula na ya biashara ili kupata uwezo wa mifuko yao.”

"Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini, haiwezekani na ili wakulima waweze kupata fedha ni lazima tuwaruhusu kufanya biashara za mazao yao pale ambapo wanaweza kuuza mazao yao,” amesema Bashe.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Kanda ya Magharibi, Emil Kasagara amesema washiriki waliojitokeza kwenye maonyesho hayo ni 232, kwamba lengo lilikuwa kupata washiriki 390.

Chanzo: mwananchi.co.tz