Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe ataka tume huru bodi ya korosho

Nafaka Bashe Bashe ataka tume huru bodi ya korosho

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Korosho Nchini (CBT) kuunda tume huru ikiongozwa na Ofisa wa usalama wa taifa kuchunguza madai ya kuwepo changamoto ambazo zinasabisha athari hasi kwenye uuzaji wa korosho ghafi nchini.

Bashe ametoa agizo hilo Novemba 27, 2023 baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wenyeviti wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma wakilalamikia changamoto nyingi ikiwemo mnada awali kuangusha bei korosho, usafirishaji wa korosho usiku na suala la utiriri wa maghala.

Amemtaka Mkurungezi wa CBT, Francis Alfred kuhakikisha tume hiyo inaundwa leo na kufanya kazi ndani ya siku 14 na kuwasilisha ripoti wizarani kwa ajili ya hatua zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu na Mkurungezi huyo, Bashe amemtaka mwenyekiti wa hiyo tume kuwa mtu wa usalama wa taifa, na baadhi ya wajumbe wakiwa ni wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

“Nataka mwenyekiti wa hiyo tume awe mtu wa Usalama wa taifa na hiyo tume ifanya kazi ndani ya siku 14,” amesema.

Amesema tume hiyo inatakiwa kuchunguza malalamiko yote ambayo yanasabisha kuanguka kwa bei ya korosho nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live