Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe apokea tani 3,100 za mbolea

Bashe Mboleaaa.jpeg Mbolea

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepokea tani 3, 100 za mbolea, akiwahakikishia wakulima hakutakuwa na upungufu wa mbolea nchini.

Akizungumza jijini hapa jana Septemba 2, wakati akipokea mbolea hiyo, Waziri Bashe amesema lengo la serikali kuja na ruzuku ya mbolea ni kuhakikisha watanzania wanazalisha chakula cha kutosha

“Tumeona katika wiki hizi za kwanza za uuzaji wa mbolea mkulima anakwenda kununua mbolea nyingi kwa hofu ruzuku hii ni ya muda mfupi

“Nataka niwahakikishie, ruzuku hii si ya muda mfupi na hatutakuwa na upungufu wa mbolea, niwatake wakulima wanunue mbolea kulingana na mahitaji yao,” amesema.

Waziri Bashe amesema hakuna haja ya wakulima kuanza kununua mifuko zaidi ya 20 kwa wakati mmoja   kwa hofu ruzuku iliyotolewa na serikali ni ya muda mfupi

“Wapo waliokuwa wakinunua mifuko 20 kwa sababu tuna mifumo yetu tukiwapigia wanatuambia ruzuku mwezi ujao inaweza isiwepo,” amesema.

Bashe amesema hakutakuwa na upungufu wa chakula kwani kipo cha kutosha na serikali itaendelea kujenga misingi ya kilimo kuwa biashara.

Kwa mujibu wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2022/23, Serikali imeongeza fedha kutoka Sh294 bilioni katika mwaka 2021/22 hadi Sh954 bilioni ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 224.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live