Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe anyooshea kidole kampuni za bia

Bashe3 Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa kilimo nchini,Husein Bashe "amezinyooshea vidole "kampuni za bia za Tanzania Breweries Ltd pamoja na Serengeti kwamba endapo watashindwa kuingia makubaliano na wakulima wa shayiri wasahau kukutana na yeye.

Bashe,alitoa kauli hiyo Jana katika kituo cha utafiti wa kilimo Tari kilichopo Selian mkoani Arusha wakati alipoenda kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho.

Akizungumza katika kituo hicho Bashe alisema kwamba mwaka 2020 kampuni hizo zilifika ofisini kwake kuomba punguzo la kodi kwa ajili ya mradi mkubwa wanaoujenga mkoani Dodoma.

Bashe,alisema kwamba wakiwa ofisini kwake kampuni hizo zilidai kuhangaikia maombi yao kwa kipindi cha miaka sita serikalini bila mafanikio na kuomba awasaidie.

Alisema kwamba kufuatia maombi hayo yeye kama waziri alivutana na wizara ya fedha kwa mwaka mmoja na nusu kupigania maombi yao mpaka yakakubalika lakini wameingia mitini.

" Tumevutana na wizara ya fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kupigania hii kesi baada ya kupata wanaleta (games)mchezo "alisema Bashe

Alisisitiza kwamba kampuni hizo zilikubali kununua shayiri kutoka kwa wakulima ambapo TBL walipanga kununua tani 6000 na Serengeti tani 2000 lakini wameenda kinyume na makubaliano.

Hatahivyo,alisema kwamba pamoja na kampuni hizo kuomba kukutana naye Mara kwa Mara lakini hatoweza kuitikia wito huo mpaka pale watakapoingia mkataba na wakulima wa shayiri.

" Wameniomba kukutana nao sitaki kuonana nao waje kwangu wakishaingia mkataba na wakulima yaani narudia they should never(wasirudie)"

"Leo wame withdraw (wamejitoa) kuingia mkataba na wakulima walisema hawajengi mpaka serikali iwape insective (nafuu) Leo serikali imewapa wanasema hawajengi" alisisitiza Bashe

Alipotafutwa meneja wa kampuni ya TBL mkoani Arusha,Joseph Mwaikasu alisema kwamba suala hilo litatolewa ufafanuzi na makao makuu.

Alipotafutwa msemaji wa kampuni ya TBL makao makuu,Mesiya Mwangoka alijibu kwa kifupi "no comment"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live