Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe akosoa Takukuru, polisi kukusanya kodi

50901 Pic+bashe

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe amekosoa utaratibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwatumia polisi, Takukuru na idara nyingine nyeti katika ukusanyaji wa kodi nchini.

Bashe alisema hayo bungeni juzi wakati akichangia makadiro ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Alisema Benki ya Dunia (WB) imetoa ripoti ya maeneo ambayo yanaisumbua Tanzania katika uwekezaji ikiwemo utitiri wa kodi ndogo ndogo.

“Leo inaanzishwa taskforce (kikosi kazi). Eti ile taskforce ina polisi wanaenda kukusanya kodi. Polisi kasomea wapi ukusanyaji wa kodi? Ina Takukuru kasomea wapi ukusanyaji wa kodi? Ina watu kutoka idara nyeti za Serikali, ina watu wa TRA.”

“Kundi hilo linakaa Kariakoo ambapo mtu akitokea na mfuko wake wanamuuliza karatasi ya ulipaji kodi kwa njia ya eletroniki, akionyesha ni feki.”

“Huyu mtu katoka Congo anajuaje kama EFDs ni feki?, anachukuliwa anawekwa Msimbazi polisi, next time (siku nyingine) haji anaenda Uganda ama nchi nyingine.”

“Ni lazima suala la ukusanyaji kodi liachwe kwa waliosomea ukusanyaji wa kodi. Polisi wakafanye kazi yao, Takukuru wakafanye kazi yao.”

Naye Mbunge Viti Maalum (Chadema), Sabrina Sungura alisema wafanyabiashara wanalalamikia mlolongo mrefu wa kodi.

“Unakuta mtu anataka kufungua ajira kwa vijana, anahitajika alipe paye (kodi ya mshahara), income tax (kodi ya mapato), Osha, manispaa, bado kuna mifuko mingi, with holding tax, fire (zimamoto), yaani ni kikwazo kikubwa,” alisema.

Alitaka kuwepo kwa mazingira rahisi kwa watu wanaotaka kufungua biashara nchini kwa kuhakikisha kuwa wanapata vibali vyote kwenye sehemu moja.

Bashe akosoa Takukuru, polisi kukusanya kodi

Sunday April 7 2019

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe akichangia

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Chanzo: mwananchi.co.tz