Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe aainisha mikakati kuukabili mfumuko wa bei

Waziri Bashe Bashe aainisha mikakati kuukabili mfumuko wa bei

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameainisha mipango ya muda mfupi na mrefu ya kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula nchini.

Amesema njia za muda mfupi ni Serikali kuuza chakula moja kwa moja kwa wananchi kupitia halmashauri husika. Njia ya muda mrefu ni mipango ya muda mrefu ni kuwekeza katika miundombinu ili kupunguza changamoto ya mazao njiani.

Bashe amesema hayo jana Jumatano Februari 8, 2023 katika mjadala kwa njia ya Twitter (Twitter Space) ulioratibiwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, uliohusu ‘Serikali imechukua hatua kukabiliana na mfumuko wa bei, nini maoni yako'.

Mjadala huo umeshirikisha wakulima, wananchi na viongozi wa Serikali akiwemo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

“Sasa hivi tumeshasambaza chakula katika mikoa 15, kwa mwezi mahindi yanayotumika nchini tani 500,000 kwa mwezi na mchele tani 90,000 za mchele.

“Serikali inapeleka chakula maeneo ambayo bei ya mahindi imevuka kati ya Sh1,200, ambapo yatauzwa kwa Sh800, hatumuuzii mfanyabiashara, bali katika vituo maalumu vya halmashuari itunawauzia wananchi,” amesema Bashe.

Amesema Serikali itaendelea kuwa imara kwa kupeleka chakula kwa wananchi, akisema changamoto ya mfumuko wa bei itapungua hadi kufikia Aprili.

“Matukio ya kupanda kwa bei ni ya muda mfupi, kuondoa tatizo hili kuongeza tija shambani ili mkulima kipato chake kishishuke,hii ndio njia bora,”amesema Bashe.

Chanzo: Mwananchi