Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe aagiza ushirikishwaji kumaliza uhaba wa mbegu kwa wakulima

BASHEEEEEEEEEEEEEEEE ED Bashe aagiza ushirikishwaji kumaliza uhaba wa mbegu kwa wakulima

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kushirikiana na wazalisha mbegu ili kutambua changamoto zao, kuhakikisha wanazifanyia kazi ikiwemo kuzifikisha Serikalini.

Waziri Bashe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wadau wa mbegu kwenye mkutano ulioitishwa na ASA jijini Dodoma ambapo amesema Serikali itaendelea kuwasikiliza na kushauriana nao kwani inatambua na kuthamini mchango wao.

Kukosekana kwa ardhi ya kuzalisha mbegu kwa wingi ni moja ya changamoto iliyowasilishwa kwa waziri Bashe katika mkutano huo.

Bashe amesema wanatakiwa kuwekana sawa kuelewana kati ya wadau, Serikali na Wakala ili kujua kwa pamoja namna ya kumaliza changamoto hiyo.

 “Hili la mashamba najibu hapa hapa kuwa siyo tatizo, cha msingi tukiwekana sawa kwani Serikali bado inayo ardhi ya kutosha ambayo tunaweza kuingia mikataba mkafanya shughuli zenu kwa urahisi,” amesema Bashe.

Mtendaji Mkuu wa ASA, Dk Sophia Kashenge amesema kuwa wamejipanga kuongeza nguvu katika uzalishaji wa mbegu bora kwa wakulima na kutengeneza bei rafiki.

Advertisement Kwa upande wake, Mbunge wa viti Maalumu, Ngwasi Kamani ameitaka Serikali kuwawezesha zaidi ASA ili waweze kuwalipa kwa wakati wazalishaji wa mbegu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live