Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe: Tunajitosheleza chakula asilimia 126

Nafaka  NAFAKA Tanzania inajitosheleza chakula asilimia 126

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa hotuba Bungeni leo Mei 17, 2022 kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Kilimo 2022/2023 na kusema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini unaridhisha kwani taifa linajitosheleza kwa asilimia 126.

"Kuhusu hali ya upatikanaji chakula, mahitaji ya chakula kwa mwaka 2021/2022 yamefikia tani milioni 14.83 ambapo tani milioni 9.44 ni za nafaka na tani milioni 5.38 ni mazao yasiyo ya nafaka"

"Mahitaji hayo ukilinganisha na upatikanaji wa tani milioni 18.66 kwa mwaka 2021/2022, Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 126"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live