Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe: Tumesambaza tani 75,282 za chakula

Nafaka  NAFAKA Bashe: Tumesambaza tani 75,282 za chakula

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo ametoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 Bungeni Dodoma ambapo amesema Wizara kupitia NFRA imesambaza tani 75,282.302 za chakula katika Halmashauri 89 zenye upungufu wa chakula na kuuzwa kwa bei kati ya Tsh. 680 hadi 920 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya soko ya Tsh. 1,200 hadi 1,500”

Akisoma hotuba hiyo Bashe amesema “Tathmini ya Kina ya Hali ya Chakula na Lishe imebaini kuwa na upungufu wa uzalishaji katika baadhi ya maeneo kwa msimu wa 2021/2022 uliotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na hivyo kusababisha kupanda bei kwa baadhi ya mazao ya chakula”

“Ili kukabiliana na hali hiyo, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency-NFRA), imesambaza tani 75,282.302 za chakula katika Halmashauri 89 zenye upungufu wa chakula na kuuzwa kwa bei kati ya Shilingi 680 hadi 920 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya soko ya Shilingi 1,200 hadi 1,500”

“Ili kukabiliana na upungufu wa chakula, Serikali inaendelea kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 506,000, aidha kwa sasa Serikali imeanza shughuli ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga miundombinu ya uhifadhi itakayoongeza uwezo wa kuhifadhi kufikia tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030”

“Lengo ni kuhakikisha kuwa, Taifa letu linauwezo wa kuhifadhi chakula cha kutumia miezi sita (6) pindi inapotokea janga ili kulinda uchumi wetu, heshima yetu, utu wetu na uhuru wetu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live