Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe: Sijahusisha udini kwenye sukari....

Sukarii Sukari Leseni Bashe: Sijahusisha udini kwenye sukari....

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kauli aliyoitoa jana Ikulu Dar es salaam kwamba Watu watarajie hadi kufikia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hali ya upatikanaji wa sukari itakuwa nzuri ilikusudia kuwa kiashiria cha muda kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha kidini kama ilivyotafsiriwa na baadhi ya Watu ambao wameikosoa kauli yake hiyo wakiihusisha na udini.

Bashe amesema “Ningependa kutoa ufafanuzi wa kauli yangu iliyonukuliwa na baadhi ya Vyombo vya Habari wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na Wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es salaam February 22,2024”

“Kama Waziri wa Kilimo, nilitoa maelezo juu ya hali ya upungufu wa sukari Nchini, na muda wa usambazaji tunaotarajia wa shehena inayofuata ya sukari, nilisisitiza kuwa kutokana na usambazaji huu na hatua tulizochukua, tutarajie hadi kufikia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hali itakua nzuri”

“Rejeo hili lilikusudiwa kuwa kiashiria cha muda kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha kidini, mara kadhaa nimesisitiza kwa kutaja vipindi vyote viwili Kwaresma na Ramadhani vina tukabili hapo mbeleni na kuwa tunajitahidi kama Serikali na azma yetu ya kutaka kutatua hii changamoto kabla ya hivi vipindi kufika na ndio maana tulianza kutoa vibali tangu mwezi wa 12, 2023, tuendelee kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo na usalama wa chakula Nchini”

Baadhi ya Watu walimuandikia maoni Waziri Bashe baada ya kuona kama amefanya udini pale alipoutaja mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan pekee bila kuitaja Kwaresma inayoendelea sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live