Menu ›
Biashara
Wed, 11 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Tanzania inategemea 20% ya Sukari inayotumika Nchini (Tani 420,000) kutoka nje, Mafuta ya Kula 60%, Ngano 90% na Mbolea 90%.
Takwimu za mwaka 2021 zilionesha Mahitaji ya Mafuta ya Kula nchini ni Tani 570,000 wakati uzalishaji ni Tani 250,000, Ngano Tani 900,000, na Mbolea Tani 700,000.
Akizungumza na Clouds TV, Waziri Bashe amesema Serikali imeweka lengo hadi kufika 2030 isiwe inaagiza Mafuta ya Kula nje lakini ana uhakika malengo yatatimia mwaka 2025.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live