Waziri Bashungwa ameeleza hayo leo Alhamisi Aprili 14, 2022 wakati akiliomba Bunge kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya zaidi ya Sh 8.77 trilioni kwa mwaka wa fedha 2022/23, akisema pia mradi huo utahusisha barabara ya Uhuru kutoka makutano ya barabara ya Mandela hadi makutano ya Mtaa wa Shaurimoyo.
“Mtaa wa Shaurimoyo kutoka makutano ya barabara ya Uhuru hadi Mtaa wa Lindi; Mtaa wa Lindi kutoka makutano ya Mtaa wa Shaurimoyo hadi kituo kikuu cha Gerezani. Kariakoo Nkurumah kutoka makutano ya barabara ya Nyerere hadi makutano ya Mtaa wa Bibi Titi na Mtaa wa Maktaba na Mtaa wa Azikiwe hadi makutano na barabara ya Kivukoni,” ameeleza Bashungwa.
Bashungwa amesema katika mwaka wa fedha 2022/23, Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) ataendelea na uboreshaji wa huduma za usafiri katika mkoani wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani ikiwa ni pamoja na kuendelea na usimamizi wa utoaji wa huduma ya usafiri wa haraka.
“Tutakamilisha taratibu za manunuzi ya mtoa huduma wa mabasi 95 ya nyongeza kwenye awamu ya kwanza ya BRT na kubadilisha mfumo wa uendeshaji na ulipaji wa watoa huduma kutoka kupokea tozo ya kupita katika mfumo wa Dart na kuanza kutumia utaratibu wa malipo ya umbali ambao mabasi yatakuwa yanatembea,” amesema Bashungwa.
Katika makadirio hayo ya bajeti, Waziri Bashungwa amebainisha kuwepo kwa ongezeko la Sh4 bilioni katika mfuko huo sawa ongezeka la asilimia 45.36 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
Advertisement