Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banio kuipatia Kibiti Sh8 bilioni kilimo cha mpunga

Wakulima Wa Mpunga Wapata Hasara Ya Mamilioni 1536x1028 Banio kuipatia Kibiti Sh8 bilioni kilimo cha mpunga

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Endapo Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti itafanikiwa kununua banio kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwenye zao la mpunga, itawaweza kukusanya Sh7.6 bilioni kwa mwaka katika zao hilo.

Hayo yamesemwa Desemba 7 na Mkurugenzi Mkuu wa mradi wa kilimo cha mpunga wa Mbakiamturi, Hamis Kambanga kwa madiwani wa Kibiti waliotembelea mradi huo uliopo Kijiji cha Kijiji cha Mtunda A wilayani humo.

Ziara hiyo imekwenda sambamba na kufanya uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2022/2023.

Katika maelezo yake kwa madiwani, Kambanga amesema uwepo wa banio hilo utawafanya kulima kilimo cha umwagiliaji na hivyo kuwa na uwezo wa kuvuna gunia 580,000 sawa na tani milioni 32,655 huku mapato ya Halmashauri yatakayopatikana yatakuwa Sh7.6 bilioni kwa mwaka.

"Tunasema mapato hayo kupatikana sababu sasa banio litatusaidia kulima mara mbili kwa mwaka na hivyo halmashauri kupata mapato makubwa zaidi.

"Kwani kilimo cha kutegemea mvua kinaua mitaji kwa kuwa ni kilimo kisichukuwa na tija na hakina uhakika na hii yote ni kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

"Hivyo mvua isiponyesha tunapoteza mtaji wote tulioingiza na hivyo kuturudisha nyuma," amesema Kambanga.

Akijibu kuhusiana na suala hilo la banio, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Msena Bina, alisema watalisukuma hilo kwenye ngazi ya Wizara kwa kuwa gharama yake sio Sh2 milioni au Sh3 milioni bali ni mabilioni yanayoongelewa.

"Naomba niseme tumeipokea changamoto hii ya banio na niahidi tutaifanyia kazi kwa kuipeleka ngazi ya juu kutokana na kuhitajika fedha nyingi kulipata ambayo ipo nje ya uwezo wa Halmashauri," amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la Madiwani, Ramadhani Mpendu, amewataka wawekezaji hao kutokatishwa tamaa kwa changamoto zilizopo kwa kuwa ni mambo ambayo yanaweza kuzungumzika.

Baadhi ya wanakijiji waliozungumzia uwekezaji huo wa zaidi ya hekari 15,000 akiwemo Mustafa Kaniki, amesema ujio wa mwekezaji huo umekuwa faraja kwao kwani walishakata tamaa katika kilimo.

Naye Mariam Mohamed amesema pamoja na mwekezaji huyo kuwalimia wanakijiji hekari zao 40 ili kuendana nao katika kilimo cha kisasa kutoka kile cha kutumia jembe, ameomba pia kuwasaidia kufikiwa na mikopo midogomidogo.

Chanzo: Mwananchi