Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Mtwara mguu sawa agizo la Rais Samia

Meli Mtwara Uturuki Bandari ya Mtwara mguu sawa agizo la Rais Samia

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bandari ya Mtwara imepokea shehena ya kontena zaidi ya 300 kwa ajili ya maandalizi ya usafirishaji wa korosho ikiwa ni utekelezaji wa agizo ambalo alilitoa Rais Samia Suluhu Septemba mwaka huu alipofanya ziara katika mkoa huu na kuagiza korosho za mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma zinasafirishwa kupitia bandari hiyo.

Akizungumza wakati akipokea kontena hizo Meneja wa Bandari Mtwara, Frednand Nyati amesema wamepokea meli yenye makontena zaidi ya 300 ikiwa ni maandalizi ya kuhakikisha shehena ya korosho inasafirishwa kupitia bandari hiyo.

Amesema kuwa kampuni nyingi zimeonyesha nia ya kuleta meli na makasha ili kuweza kubeba mzigo wote wa korosho ambapo Novemba tunarajia kupokwa zaidi ya meli saba zitakazokuwa na makasha 400 kwa kila meli ambapo Desemba pia zitakuja nyingine.

"Ili kuhakikisha tunatekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu ya korosho zote kusafirishwa kupitia bandari ya Mtwara tumejipanga kwenye vifaa na Serikali imeshaleta mitambo mingi mikubwa ambayo tunaimani kuwa itasaidia kuharakisha usafirishaji na ufanisi mkubwa kusafirisha korosho,"amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa ujio wa kontena hizo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu ili kuhakikisha kuwa shehena yote ya korosho inasafirishwa kupitia bandari ya Mtwara.

"Rais alipokuwa ziarani mkoani hapa alitoa maelekezo na maagizo juu ya usafiishaji wa korosho leo tunashuhudia makasha yakija kwa meli kwaajili ya kubeba korosho ambapo tunaaamini kuwa usarishaji sasa utaanza na kuchagiza ufanyaji wa bishara ndani ya mkoa wetu" amesema Munkunda

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mkuu wa Bodi ya KoroshoTanzania, Revelian Ngaiza amesema kuwa minada imeanza ambapo mpaka jana tani 20,000 zilikuwa zimeuzwa katika minada mine huku mwitikio wa wakulima kukusanya korosho ni mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live