Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Mtwara inavyobebwa na shehena ya korosho

Thu, 13 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Korosho ndiyo shehena inayoibeba bandari ya Mtwara kwa asilimia 60, amesema meneja wa bandari hiyo, Nelson Malali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Desemba 12, 2018 waliotembelea bandari hiyo,  Mlali amesema kwa mwaka 2013/14 walihudumia  tani 356,356 kwa ujumla ikiwemo na Korosho.

"Mwaka 2014/15 tukashuka kwa kuhudumia tani 296,577 halafu mwaka uliofuatia 2015/16 tukashuka tena kufikia tani 268,035 halafu tukapanda tena kufikia 377,590,"amesmea Mlali.

Amesema shehena ilipungua kwa miaka hiyo miwili kwa kuwa uzalishaji wa korosho ulipungua ndiyo maana hali ikawa hivyo.

"Asilimia 60 matumizi ya bandari ya  Mtwara katika shehena ni korosho," amesema.

Amesema ili kukabiliana na hali hiyo pale uzalishaji unaposhuka bandari hiyo inafanyiwa upanuzi ili iweze kuhudumia shehena kubwa inayotokana na viwanda nchini hasa vilivyopo kusini.

Amesema ujenzi wa gati yenye upana wa mita 350 na  urefu wa mita 13 utasaidia kuhudumia tani 65,000 kwa kuwa kwa gati lililopo sasa hivi ni meli moja tu kubwa inayoweza kuhudumiwa.

"Gati hilo litaanza kutumika mwakani(2019) na tukiona Meli nyingi ziko Dar tutaomba zihamishiwe hapa kwa kuwa kuna nafasi,” amesema.

Amesema kwa hivi sasa ongezeko la meli kubwa inakuwa  kwa  asilimia 36 lakini zamani ilikuwa chini ya asilimia 30 na mapato kwa sasa ni asilimia 19 kutoka 9.



Chanzo: mwananchi.co.tz