Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Kilwa kutengeneza ajira 30,000

Bandari Kilwa Bandari ya Kilwa kutengeneza ajira 30,000

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amesema mradi wa ujenzi wa bandari ya Kilwa Masoko mkoani Lindi utaajiri vijana wasiopungua elfu 30.

Waziri Ulega ametoa kauli hiyo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bandari ya uvuvi Kilwa Masoko.

“Bandari hii itaajiri vijana wasiopungua elfu thelathini na miongoni mwa vijana hao watatoka Kilwa, Lindi na maeneo mengine yote ya Taifa letu". amesema Waziri Ulega

Bandari ya Kilwa Masoko itakuwa na eneo la kuhifadhia samaki ambapo kutakua na maeneo mawili moja la kuhifadhi samaki walioganda na eneo la pili ni samaki ambao hawajaganda na ndani ya bandari kutakua na soko la samaki ambalo litatumika na wavuvi wa Kilwa na wavuvi kutoka sehemu nyingine.

Pia kutakuwa na eneo la kuchakata samaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live