Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Dar yapanda viwango

BANDARIII Bandari ya Dar yapanda viwango

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeridhishwa na kasi ya utekelezaji na usimamamizi wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, unaotekelezwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya kamati yake kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya serikali iliyotekelezwa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso amesema kamati yake imeridhishwa na kasi kubwa katika utekelezaji wa mradi wa maboresho ya bandari hiyo.

“ Kamati inaendelea kuishukuru serikali kwa mradi huu wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, kuna mabadiliko makubwa yameonekana. Tunaishauri serikali, mradi huu ukamilike kwa muda uliopangwa, ili bandari iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” amesema Kakoso.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi , Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya maboresho ya bandari nchini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya bandari.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Elihuruma Lema, amesema mradi wa kimkakati wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam umefikia asilimia 90, ikihusisha eneo jipya la kupokelea magari - RoRo, maboresho ya gati namba 1 hadi 7, eneo la kupokelea makasha, kutanua lango na kuongeza kina cha maji cha eneo la kugeuzia meli na ununuzi wa mashine na vitendea kazi mbalimbali vya kuhudumia shehena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live