Bandari ya Dar Es Salaam sasa itakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa baada ya shilingi bilioni 9.8 kutumika katika kuiboresha.
Awali bandari hiyo iliweza kupokea meli tano hadi sita lakini kwa sasa inaweza kupokea meli 12 na kushusha mizigo kwa siku tano kwa tani 45,000 ilikinganishwa na siku 10 hadi 11 za awali kwa tani 40,000.
Akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, Mkurugezi wa Bandari hiyo Elihuruma Lema amesema uboreshaji huo umefikia asilimia 98 hadi sasa.
“Kazi kubwa ilikuwa kuboresha magati kuanzia namba 0 ambalo halikuwepo na sasa tumetengeneza lakini tumetengeneza gati na hili nyuma ilikuwa ni kina cha mita 8.5 baada ya maboresho tumeongeza imekuwa mita 14.5 na ikaimarishwa kuingai ndania mita 15 ya gati.
“Hii Inamaanisha kuwa uwezo wa bandari umeeongezeka awali tulikuwa tunahudumia meli sita kuanzia gati 1 hadi 7 lakini sasa kuanzia 0 tunaweza kuweka meli 12 kwa wakati mmoja mizigo kama mizigo ya magari ,mafuta na kontena zimeongezeka,”alieleza.
Amesema wiki mbili zilizopita walipokea meli kubwa ya historia kwa Afrika Mashariki ambayo ilibeba magari 3743 kwa mara moja.
“Sasa awamu inayofata ni upanuzi wa lango la kuingia meli lina mita 11.5 upanuzi ukimalizika itakuwa na mita 15.5 meli kubwa zaidi zitaingia zenye zaidi ya mita 200 mpaka 400 na kuna eneo la kupaki magari ambalo lina mita 72,000,”amefafanua Lema.