Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Dar inahudumia meli 200 kwa mwezi

Wabunge EALA Wahadharisha Ubaguzi Uwekezaji Wa Bandari Bandari ya Dar inahudumia meli 200 kwa mwezi

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema kutokana na maboresho ya bandari meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja, hivyo kupelekea wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja, kutoka meli 70 ndani ya mwezi mmoja.

Akizingumza katika mkutano wa TPA na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mbossa amesema ongezeko la meli limetokana na maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, kampeni za kimasoko, kuonana ana kwa ana na wateja wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuimarika kwa diplomasia ya uchumi.

Pia, amesema kutokana na mikakati mbalimbali ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kumepelekea kuwepo kwa ujenzi wa miradi mingi na hivyo kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mizigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live