Menu ›
Biashara
Wed, 25 Oct 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rais Samia Suluhu Hassan ameisihi serikali ya Zambia na jumuiya ya wafanyabiashara nchi humo kutambua kuwa milango ya ushirikiano na uwekezaji katika eneo la bandari inaendelea kuwa wazi.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Zambia ambayo yeye ndiye mgeni rasmi ambapo viongozi wote wawili wamegusia uhusiano mzuri na ushirikiano uliopo kwenye biashara tangu enzi za Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Keneth Kaunda
Uhusiano huo unaoendelea kuimarishwa siku hadi siku umepelekea kuanzishwa kwa miundombinu ya pamoja ambayo ni TAZARA, TAZAMA na TANZAM.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live