Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari Dar yaweka historia ikipokea meli ya KMTC

AU, Somalia Na Ethiopia Wakutana Kuhusu Mzozo Wa Bandari Bandari Dar yaweka historia ikipokea meli ya KMTC

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara amesema Bandari ya Dar es Salaam ipo tayari kupokea meli kubwa za mizigo kutoka mataifa mbalimbali kutokana na maboresho yaliyofanyika ambayo yameongeza ufanisi katika kuhudumia shehena za mizigo.

Kiongozi huyo ameyasema hayo jana mara baada ya kupokea meli ya mizigo ya Shirika la KMTC kutoka China, ikifanya safari zake moja kwa moja kutoka nchini humo hadi Tanzania ikiwa na makasha 1,500.

“Tunajivunia sana kazi inayofanyika hapa, tunaona mabadiliko makubwa kwa kuwa tumepokea meli iliyotoka China moja kwa moja. Uwezo wetu kuhudumia shehena ni mkubwa na wenye ufanisi mzuri,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema kutokana na maboresho yaliyofanyika bandarini hapo, sasa inahudumia shehena kubwa ya mizigo kutokana na wingi wa meli zinazotia nanga kila siku.

Bandari ya Dar es salaam inakuwa ni ya kwanza Afrika kwa meli ya Shirika la KMTC kutia nanga ikiwa imebeba mzigo wa makasha 1,500.

KMTC (Korea Marine Transport Co. Lts) ilianzishwa mwaka 1954 ikiwa ni kampuni kiongozi katika ubeba mizigo kwa usafiri wa majini kutoka bara moja hadi jingine.

“Kwa miaka 60 tumekuwa watoa huduma bora kati ya Asia na masoko ya India pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika ya Kati. Mwaka 2022 KMTC ilikuwa ni kampuni namba moja ikiwa na hisa Korea, Japan na Kusini mwa Asia ikiunganisha bandari za kimataifa 90 katika nchi 25,”ilifafanua taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live