Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari DSM wafunga mtambo wa kubaini wizi wa mafuta

Bandari Serikali kudhibiti wizi wa Mafuta Banddari

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla , ameshuhudia na kukagua kifaa cha kisasa cha kubaini wizi na upotevu wa mafuta ghafi (radio detector) kutoka bomba kuu la kupokea mafuta kwenye meli kuelekea kwa wafanyabiashara ambapo kifaa hicho kinatarajiwa kuanza zoezi la ukaguzi muda wowote kuanzia leo.

Upatikanaji wa kifaa hicho ni kufuatia maelekezo aliyotoa , Mkuu huyo wa Mkoa, kwa TPA baada ya kuunda kamati ya ufuatiliaji upotevu wa mafuta ambapo miongoni mwa mapendekezo ya kamati ilikuwa ni ununuzi wa kifaa cha kudhibiti wizi wa mafuta bandarini.

Aidha, Makalla amewahakikishia wafanyabiashara wa mafuta kuwa Serikali imejidhatiti kumaliza kabisa tatizo la upotevu wa mafuta na anashukuru kuona hadi sasa kumekuwa na matokeo mazuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live