Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari DSM kuhudumia hadi tani milioni 20

Bandari Ya Dar.jpeg Bandari DSM kuhudumia hadi tani milioni 20

Mon, 29 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bandari ya Dar es Salaam inatarajia kuvuka lengo katika kuhudumia shehena za mizigo inayowasili kupitia bandari hiyo hadi kufikia tani Milioni 20 kutoka Tani Milioni 19.6 kwa mwaka huu wa fedha wa 2022/2023.

Akitoa maelezo ya maendeleo ya mradi huo wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam yatakayogharimu takribani shilingi Bilioni 421 hadi kukamilika kwake, Mkurugenzi wa bandari ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amesema, maboresho yanayoendelea yameiwezesha bandari hiyo mpaka sasa kuhudumia shehena za mizigo zaidi ya tani Milioni 18 .

Ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha ujao wa 2023/2024, bandari ya Dar es Salaam inalenga kuongeza uwekezaji kwenye vifaa vya kisasa vya kuhudumia shehena za makasha vinavyotumia teknolojia ya Ship to Show Ganti Train (SSG), yenye uwezo wa kuhudumia makasha 35 kwa saa ambapo itaongeza ufanisi wa utoaji wa mizigo kufikia makasha zaidi ya elfu tano kwa siku.

Mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam umehusisha utanuzi wa lango la kuingilia meli, eneo la hifadhi ya magari na uboreshaji wa magati ili kuwezesha meli zenye ukubwa wa Mita zaidi ya 300 kutia nanga bandarini hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live