Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari Bubu nchini zafika  693

A51746ed2dc2dd0a684a7a1edc0fab7e Bandari Bubu nchini zafika  693

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya bandari nchini(TPA) imesema kutoka na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo umegundua ongezeko la bandari bubu nchini imefikia idadi ya 693.

Tafiti hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TPA, Bi. Leticia Mutaki wakati alipokuwa akizungumza na wamiliki wa bandari pamoja na watumishi wa mamlaka yao wakati wa kikao cha mkutano kazi.

Alisema Ziwa Victoria ni kinara wa bandari bubu ambapo zipo 329 huku ikifuatiwa na Dar-es-salaam yenye bandari bubu 116 kisha Ziwa Tanganyika zipo 108.

Alisema Mtwara ina bandari bubu 73,Tanga zipo 50 na ziwa Nyasa zipo 17. Alisema kuongozeka kwa uchumi kumepeleka ongezeko kubwa sana la bandari bubu.

Alisema Mamlaka yao itakagua bandari hizo na kujua ni aina gani ya shughuli zinazofanyika. Alisema katika Ziwa viktoria bandari zinazotambulika ni Mkombozi,Kamanga,Nile perch fisheries na Nyehunge.

Akielezea kuhusu maboresho ya sheria ya Bandari ya mwaka 2004,alisema sheria mpya inataka kushirikisha wadau kuhusu uendeshaji wa bandari na inavifungu vinavyoonyesha majukumu ya bandari.

Alisema sheria mpya hairuhusu meli zetu kutia Nanga popote bali meli inatakiwa kutia nanga sehemu rasmi ambayo ni bandari.

Meneja msaidizi wa huduma ya bandari(TRA),Oswald Massawe ameiomba mamlaka ya nchini Bandari(TPA)kuangalia jinsi ya kurasimisha bandari hizo kwakuwa serikali inapoteza mapato mengi sana.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Nyehunge Express,Anwar Said alisema maboresho ya sheria mpya itawasaidia kumiliki bandari kwa vigezo malumu na kufanya shughuli zao bila usumbufu.

Alisema kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya urasimishaji kwakuwa wamekuwa wakilipia mapato makubwa sana.

Chanzo: habarileo.co.tz