Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BancABC yawapa ‘dili’ wanawake wafanyabiashara Tanzania

32343 NEMKIPIC Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. BancABC Tanzania imewafumbua macho wanachama wa  Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) katika mkutano wa mwezi wa chama hicho baada ya kuwaeleza jinsi watakavyopata urahisi wa kubadili fedha wanapokwenda China katika biashara.

Mkutano huo uliwakutanisha zaidi ya wanachama 250 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kuzungumzia maendeleo na changamoto zinazowakabili.

Akizungumza katika mkutano huo, mkurugenzi wa kitengo cha Dijitali wa benki hiyo, Silas Matoi amesema wanatambua umuhimu wa wanawake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amesema benki hiyo imeweka mikakati ya kuendelea kuwawezesha wanawake huku akibainisha jinsi wanachama wa TWCC wanavyokumbana na vikwazo wakienda China, hasa kubadilisha fedha.

“BancABC  ina suluhisho la jinsi ya kupata fedha za kigeni mnapokuwa katika safari China. Tuna kadi ya malipo ya kabla ya  ‘YUAN pre-paid Visa card’, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China,” amesema.

“Kadi hii maalum inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za China kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza  changamoto za kubadilisha fedha ambazo nyinyi wafanyabiashara huwa mnazipata.”

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa TWCC,  Mwanjuma Hamza amesema, “Lengo letu ni kufanya wanawake wakue kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kushiriki maonyesho kadhaa ya biashara ndani na nje ya nchi.”

“Kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu wanawake wanachama wa TWCC walishiriki kwenye maonyesho kuanzia ngazi ya mkoa, Taifa na kimataifa na hivyo kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao kutoka na ujuzi wanaoupata.”

 



Chanzo: mwananchi.co.tz