Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi amulika fursa za biashara Zambia

Balozi Zambiaa Zambiaa (600 X 377) Balozi amulika fursa za biashara Zambia

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo nchini humo.

Balozi Mkingule ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, aliyetembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini, Zambia.

Amesema baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Waasisi wa Tanzania na Zambia, jukumu lililopo kwa sasa ni kujielekeza katika ukombozi wa kiuchumi.

Balozi huyo wa Tanzania nchini Zambia amewahakikishia Wawekezaji wa Tanzania kuwa uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa hayo mawili umefungua milango ya uwekezaji na biashara.

Amesema ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia ipo tayari kuwasaidia Wafanyabiashara wa Tanzania watakaokuwa tayari kuwekeza Zambia.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amempongeza Balozi Mkingule kwa jitihada zake za kuwaunganisha Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia na amewapongeza Wafanyabiashara ambao wameanza kuchangamkia fursa zilizopo Zambia.

Aidha, Msigwa ambaye ametembelea jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia ambalo lilijengwa tangu mwaka 1971 amesema, Serikali imeanza mchakato wa kujenga majengo ya kisasa katika nchi mbalimbali zenye Balozi za Tanzania ikiwemo Zambia ili yaendane na hadhi ya Tanzania.

Msigwa na Maafisa Uhusiano wengine kutoka Tanzania wapo nchini Zambia kuhudhuria mkutano wa Maafisa Uhusiano Barani Afrika ambao kesho Mei 16, 2023 Rais Hakainde Hichilema wa Zambia atahutubia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live