Katika #TembeaNaBajeti leo, Mwananchi Digital imezungumza na Godfrey Mramba, mtaalamu wa kodi na Mkurugenzi Mtendaji (Managing Partner & CEO) wa Basil & Alred, kuhusu jinsi ambavyo mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018/19 yatakavyochochea uchumi shirikishi, kwa kuwanufaisha wananchi katika maisha yao ya kila siku.
Je ana mtazamo gani kuhusu malengo ya serikali? Nafuu utaipata wapi? Je, punguzo za kodi mbalimbali zitakunufaishaje mwananchi wa kawaida? 2018/19, mfuko wako utatuna, ama utanyong'onyea? Tazama video kujua zaidi...
KUHUSU Basil & Alred:
Basil & Alred ni kampuni ya kitaalamu inayotoa huduma za ushauri na mikakati ya kodi na bima, na ushauri wa kibiashara iliyoko jijini Dar es Salaam.
Uongozi na wataalam wa Basil & Alred wana ufahamu wa kina wa sekta mbalimbali nchini, ikiwamo bima, benki, mawasiliano, mafuta na gesi, madini, viwanda, kilimo, biashara na usafirishaji. Kujua zaidi, watembelee hapa: http://basilalred.com/