Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba, Mtoto marubani Air Tanzania

25f304a77712ce62bfa2968a942e0d21 Baba, Mtoto marubani Air Tanzania

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIKA hali isiyotarajiwa lakini ndiyo ukweli ni kuwa marubani wawili wanaorusha ndege za Air Tanzania ni baba na mtoto wake.

Katika ufafanuzi wake, Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania (ATCL) ilisema kuwa “Tunajivunia kuona kwenye timu yetu kuna baba na mtoto wake na wote wanarusha ndege zetu za Air Tanzania, hii ni mara ya kwanza kwenye historia yetu kwa baba na mwanae kuwa marubani wetu...

"Capt. Arif Jinnah amekuwa rubani kwa miaka 33 anarusha Airbus A220 na mwanae Amour Arif amejiunga nasi kama Ofisa wa kwanza (co-pilot) kwenye timu ya Bombardier Q400 na ndiye rubani mdogo zaidi wa Air Tanzania akiwa na miaka 21 pekee,” ilisema kampuni hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz