Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baadhi ya mabasi ya abiria yaanza kuchukua tahadhari ya corona

99415 Pic+mabasi Baadhi ya mabasi ya abiria yaanza kuchukua tahadhari ya corona

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baadhi ya mabasi ya mikoani yameanza kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi vya corona kwa kuwasafisha abiria wao mikono kwa kutumia dawa maalumu (sanitizer) kabla ya kuingia ndani ya basi.

Hata hivyo, mabasi mengi bado hayajachukua tahadhari zozote, abiria wanakata tiketi na kuingia kwenye basi kama kawaida na tahadhari dhidi ya ugonjwa huo inabaki juu ya abiria mwenyewe.

Mwananchi imeweka kambi leo Jumatano, Machi 18 katika kituo cha mabasi cha Ubungo na kubaini mwitikio mdogo wa tahadhari zinazotolewa hasa maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.

Kondakta wa basi la Kimbinyiko linalofanya safari zake za Dar - Dodoma, Nassor Mohammed amesema wao wamezingatia tahadhari za ugonjwa wa corona na wanawalinda abiria wao kwa kuwanyunyizia dawa ya kuua wadudu mikononi. "Hili jambo ni kubwa na Serikali imekuwa ikituhamasisha kuchukua tahadhari. Tunashukuru viongozi wetu wametupa hizi maski na sanitizer kwa ajili ya kila abiria anayeingia kwenye basi," amesema Mohammed ambaye alikuwa amevaa maski.

Kondakta wa basi la ABC International, Jonathan Kikoti amesema wanatambua athari za ugonjwa wa corona na jinsi ulivyoua watu wengi, hivyo, wameona nao wajikinginge kwa kutumia sanitizer na barakoa(maski).

"Hapa mlangoni tunawanyunyizia abiria dawa, na huko ndani baadhi yao wamevaa mask kama sisi lakini wengine hawana. Tumewatangazia kuchukua tahadhari kama vile kutopeana mikono," amesema Kikoti. Hata hivyo, kondakta wa basi moja ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameulaumu uongozi wake kwa kutochukua tahadhari zozote kama ilivyo kwenye mabasi mengine.

Katika jengo la abiria, ndoo ya maji ya kunawa imewekwa na kila abiria anayeingia anaambiwa "kunawa mikono bure". Baadhi ya wafanyabiashara katika stendi ya mabasi ya Ubungo pia wamevaa barakoa na glovu mikononi.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz