Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baadhi ya bidhaa kuanza kushuka bei nchini

Bei Za Bidhaa 4.crdownload Baadhi ya bidhaa kuanza kushuka bei nchini

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: eatv.tv

Serikali imesema vipo viashiria vya kuonesha ukuaji wa hali ya uchumi nchini, huku ikielezwa kuwa baadhi ya bidhaa zitaanza kushuka bei mara baada ya bidhaa muhimu kushuka ikiwemo nishati ya mafuta.

Kauli hiyo imetolewa hii Septemba 14, 2022, na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya Dunia kupitia MIGA kitengo ambacho kinawahakikishia wawekezaji kuwekeza nchi mbalimbali za Afrika ambapo Tanzania imetajwa kama nchi ambayo kwa sasa imejipambanua katika kufungua milango yake Kwa ajili ya wawekezaji kuingiza mitaji yao kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na utalii.

Mkutano huo umewahakikishia wawekezaji kutumia fursa zilizofunguliwa na serikali kufika kutengeneza fursa za ajira na kuongeza kipato.  

Chanzo: eatv.tv