Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya zabibu, Dodoma kulima pamba, korosho

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Katika kutekeleza azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati unaotokana na viwanda ifikapo 2020, mkoa wa Dodoma umeanza kulima mazao ya pamba na korosho kama mazao yao ya kimkakati.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Desemba  18, 2018 na ofisa kilimo wa mkoa huo, Bernard Abraham wakati akiwasilisha maendeleo ya kilimo ya mkoa huo na kubainisha kuwa Dodoma inategemea shughuli za kilimo kwa asilimia 72.8.

Amesema mkoa wa Dodoma una hekta 2.1milioni zinazofaa kwa kilimo lakini mpaka sasa hekta zilizotumika ni 1.0milioni sawa na asilimia 47 ya eneo lote linalofaa kwa kilimo.

Ametaja mazao mengine ya kimkakati yanayolimwa katika mkoa huo kuwa ni alizeti na zabibu japo bado kuna changamoto kubwa ya kupata mbegu bora za mazao yanayostahimili hali ya hewa ya mkoa huo.

Amesema kwa mwaka 2017/18 Dodoma ilijiwekea malengo ya kuvuna tani 1.8 za mazao lakini waliweza kuvuna tani 1.2 tu na kushindwa kufikia lengo.

Kwa upande wake mbunge wa Chemba, Juma Nkamia ameutaka mkoa huo kutoa elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha zao la pamba kwa kuwa wananchi wanaweza wakaacha kulima mazao mengine ya chakula na kuhamia kwenye zao hilo na kusababisha njaa kubwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz