Tajiri namba moja duniani, Elon Musk, amesema anajipanga kuinunua kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola akiahidi kurejesha cocaine kwenye kinywaji hicho.
Musk aliandika Aprili 28 kwenye ukurasa wake wa Twitter “Next I’m buying Coca-Cola to put the cocaine back in.”
Kwa muda mrefu, Coca Cola imekuwa ni bidhaa kubwa ikitambulika nje ya mipaka ya Marekani. Kulingana na Jarida la Scientific American, kiungo cha asili cha kinywaji hicho kilihusisha cocaine.
Hata hivyo inadaiwa soda hiyo bado ina kiasi fulani cha majani ya koka ambayo hutumika kuzalisha unga haramu mweupe unaotambulika kwa majina kama pele, diego, white sugar na sembe.
Tweet ya tajiri huyo hadi jana mchana ilikuwa na likes milioni 2.8, lakini vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa kauli ya Musk ni utani kama ilivyo desturi yake, wala sio suala lenye uhalisia kwamba anapanga kuinunua kampuni hiyo.