Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya December 9 ujenzi Kariakoo mpya kuanza

Screenshot 2021 12 02 At 16.02.50 660x400.png Baada ya December 9 ujenzi Kariakoo mpya kuanza

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amesema ukarabati wa Soko la Kariakoo lililoungua na Ujenzi wa Soko jipya la Ghorofa 6 utaanza baada ya December 09 baada ya Mkandarasi kupatikana.

RC Makalla amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Tsh. Bilioni 2 kwa vikundi vya ujasiriamali ambapo amesema tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Tsh. Bilioni 28 kwa ajili ya ujenzi huo.

RC Makalla amewaondoa hofu Wafanyabiashara wa Soko hilo wenye wasiwasi kuwa baada ya ujenzi kukamilika watapangishwa Watu wengine ambapo amesema Wazawa watapewa kipaumbele.

Chanzo: millardayo.com