Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baa, kumbi za sherehe zilizopigwa 'stop' kufunguliwa

Baa Bar Kumbi Baa, kumbi za sherehe zilizopigwa 'stop' kufunguliwa

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeanza kuzifungulia baa na kumbi za starehe ambazo zimekidhi matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 ambayo pamoja na mambo mengine, imeweka kiwango cha mitetemo ya sauti.

Kwa Mujibu wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo, hadi kufikia leo, Jumanne, kumbi baa tano zilizofungiwa jijini Dodoma zimeshafunguliwa na tayari nne zimeshaanza kazi baada ya kukidhi matakwa ya Sheria hiyo.

Dk Jafo amelazimika kutoa maelezo hayo Bungeni, Dodoma leo asubuhi baada ya Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ kuomba mwongozo kupitia Kanuni ya 54(1) akieleza kuwa taifa linakosa mapato kwa kufungwa kwa maeneo hayo.

Aidha, Musukuma amesema Watanzania wanashauriwa kupata muda wa kujiburudisha na si kujifungia ndani.

Baada ya kumsikiliza, Naibu Spika Musa Azan ‘Zungu’ alimtaka Dk Jafo kuelezea suala hilo.

“Kulikuwa na malalamiko…watoto wanapoteza usikivu, wagonjwa wanapoteza maisha. Hatujui ni akina mama wangapi wamepoteza ujauzito kutokana na kelele.

“Wengi wameanza ku-comply [kukidhi matakwa ya Kisheria] baa zote zitafunguliwa. Tumeweka utaratibu mzuri,” Waziri ameliambia Bunge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live