Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BRELA yawataka Wafanyabiashara kujisajili

BRELA Yawataka Wafanyabiashara Kujisajili BRELA yawataka Wafanyabiashara kujisajili

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: dar24

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini – BRELA, imewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujisajili kwani wasio na usajili hawatoweza kuomba tenda rasmi ambazo zinatangazwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na Idara zake.

Hayo yalisemwa na Afisa Sheria wa BRELA, Lupakisyo Mwambiga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga.

Alisema, ni vema Wafanyabiashara na Wajasiriamali wakaona umuhimu wa kurasimisha biashara zao kwa kusajili brela na kupata leseni inayostahili ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara.

“Wengi wanachanganya leseni kati ya daraja A na B ambazo zinatolewa na halmashauri na Manipsaa kuna biashara zenye sura ya kitaifa na kimataifa unatakiwa kupata leseni kutoka brela hivyo nawahimiza wafanyabishara waje kupata elimu kwa kueleza biashara wanazofanya,“ aliongeza Mwambiga.

Ofisa Sheria kutoka BRELA, Lupakisyo Mwambinga wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Aidha, aliongeza kuwa kuna leseni ya uanzishwaji wa kiwanda na leseni biashara kwa wajasirimali wenye viwanda vidogo na wafanyabiashara wenye viwanda vikubwa huku akiwataka kutembelea banda lao ili waone ni vitu gani wanaweza kufanya kupata leseni.

Hata hivyo, Mwambiga alisema wapo kushiriki kwenye maonyesho ya biashara na utalii kutokana na kwamba ni moja ya taasisi za kusimamia usajili wa biashara pamoja na leseni na wamekuja kutoa elimu na huduma za papo kwa papo ikiwemo usajili wa kampuni ,majina ya biashara.

BRELA inatumia maonesho hayo kutoa leseni kundi A na utoaji wa leseni za viwanda na usajili wa alama za biashara kwa wateja wao huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza kufika kwenye banda lao ili wawez kupata ushauri jinsi gani wanaweza kusajili kampuni, jina la biashara au alama ya bisharaa.

Aidha, walio tayari wanasajiliwa kupitia mtandao kwa kuwasaidia kwa sababu wapo kwenye maonyesho na wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara umuhimu wa kusajili au kurasimisha biashara maana wengi mpaka wakipata changamoto Fulani ndio wanakilimbia brela.

Chanzo: dar24