Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BRELA kukabiliana na Rushwa Utoaji wa Leseni.

Brela Mkurugenzi Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) sasa, wataanza kutoa Leseni za Biashara kwa njia ya Kielektroniki kama moja ya jithada zinzofanywa na Brela katika kukabiliana na Rushwa ndani ya taasisi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa alisema kumekuwepo na baadhi ya wafanyakazi ambao hutoa huduma hiyo kwa rushwa na kutumia njia zisizo halali kutoa leseni na kuikosesha serikali mapato.

Bwan.Nyaisa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo wafanyakazi katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Morogoro.

"Mfumo mpya wa kutoa leseni kwa njia ya kielekroniki utasaidia kuepusha kuwakutanisha Maafisa Biashara na wateja ana kwa ana, na kuepusha tatizo la rushwa iliyokithiri ndani ya BRELA" amesema Nyaisa.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuwapitisha washiriki kwenye sheria ya leseni ya biashara itawajenga wafanyakazi katika kutambua majukumu yao kwenye usajili na kutambua mipaka kati yao na mteja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live