Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BIASHARA KUJIONGEZA !! Bajaji ya Dar yenye free Wi-Fi

1823 Bajaji 660x400

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Ayo TV na millardayo.com kwenye pitapita zake mjini imekutana na kufanya mahojiano na kijana anayejulikana kwa jina la Peter mwenye miaka 25 ambaye ni dereva wa bajaji ambaye kituo chake cha kazi ni Victoria, jijini Dar es Salaam.

Kitu cha kufurahisha na kinachomtofautisha kijana huyo na waendesha bajaji wengine ni jinsi alivyoongeza ubunifu kwenye biashara yake kwa kuweka Wi-Fi ya bure kwaajili ya wateja wake.

Huduma hiyo ya Wi-Fi katika bajaji haiongezi gharama yoyote katika bei zake na ameeleza kuwa nia yake ilikuwa ni kuvutia wateja, ukizingatia jiji la DSM lilivyo na foleni, Wi-Fi inawasaidia wateja wake kuendelea kupata internet wakiwa kwenye foleni.



Aunt Ezekiel azua gumzo na maswali “dahh! Wanaumeā€¯



Asante Mungu haikutokea ajali…. Madereva wote wawili wanashughulikiwa



 

Chanzo: millardayo.com