Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BBT kielelezo kilimo cha Tanzania

Wadudu Dawa Kilimo BBT kielelezo kilimo cha Tanzania

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amesema hatua zinazochukuliwa na nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwa na uhakika wa chakula zinaonesha matumaini kuwa ukanda huo uko tayari kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akizungumza mkoani Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa juu unaohusisha pia Marais na Wakuu wengine wa Serikali wa Ukanda huo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi na uhakika wa chakula Desalegn amesema, mpango wa Jenga kesho Bora (BBT) unaotekelezwa na Tanzania ni kielelezo cha nchi hiyo ilivyojiandaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuwa na uhakika wa chakula.

Desalegne amesema, mpango huo wa BBT unaonesha kuwa Tanzania inajiandaa kuwa na chakula cha uhakika bila kujali mabadiliko ya tabianchi ambayo yataathiri pia upatikanaji wa chakula kwenye nchi nyingi duniani.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Ethiopia pia amesema, jitihada zinazofanywa na nchi ya Rwanda katika kubadili ardhi yake ya milima kuhimili kilimo inaifanya nchi hiyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa na uhakika wa chakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live