Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10 na 8703.80.90 na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini (engine capacity) kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee yanayotambulika kwa HS Code 8702.40.11; 8702.40.19; 8703.80.10 na 8703.80.90 na magari yanayotumia Nishati ya Gesi Asilia (CNG) pekee. “Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni inayotumika kuagiza nishati ya mafuta kutoka nje ya Nchi”