Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azim Dewij: Kufanya biashara halali ni ibada

AZIM DEWJ Azim Dewij: Kufanya biashara halali ni ibada

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara maarufu nchini Azim Dewji ametoa rai kwa Wafanyabiashara nchini kuuza bidhaa kwa bei nafuu kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwani imekuwa kawaida baadhi ya bidhaa kupanda bei kila kinapofika kipindi hicho cha mwaka.

"Bahati mbaya sana kwenye baadhi ya maeneo wanaopandisha bei za bidhaa ni Waislamu wenyewe, mimi nawaomba sana ndugu zangu Wafanyabiashara kutoka dini zote mwaka huu tuonyeshe mfano tuuze bidhaa kwa bei elekezi," Amesema Azim Dewji

Ameyasema hayo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi na Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir alipopata nafasi ya kutoa salamu katika shughuli ya Dua ya kuwaombea Masheikh wa Tanzania iliyofanyika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni, Dar es Salaam ambapo Rais Mwinyi alikuwa mgeni rasmi.

Amesema kufanya biashara halali ni ibada na kujitolea kuuza bidhaa kwa bei elekezi/nafuu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni sawa na kufuturisha maelefu ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live