Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso ajibu kilio cha wavuvi Pangani

Aweso 25 At 15.jpeg Aweso ajibu kilio cha wavuvi Pangani

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Kata ya Mkwaja Wilayani Pangani mkoani Tanga wamemuomba Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso kwa kushirikiana na Serikali kupatiwa Boti ya Uokoaji itakayo wasaidia wavuvi katika eneo hilo kufanya Shughuli za Uokoaji pindi yanapotokea majanga

Akijibu Kilio cha wananchi hao katika Mkutano uliofanyika katika eneo hilo akiambatana na Kamati ya Siasa Wilaya ya Pangani, Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la hilo Jumaa Aweso ameahidi kutoa Tsh Milioni 11 kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itakayoenda kununua Boti ya Uokoaji kwa wavuvi hao

Aidha Waziri Aweso amewaonya Wananchi hao juu ya Fedha zitakazotolewa kwa ajili ya Ununuzi wa Boti hiyo ambapo amesema asitokee mtu yoyote akatumia fedha hizo vibaya, na badala ya fedha hizo zikatumike kama zilivyokusudiwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live