Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atakayekwamisha Wafanyabiashara kuchukuliwa hatua

Wafanyabiashara Watakaowakwamisha (600 X 365) Atakayekwamisha Wafanyabiashara kuchukuliwa hatua

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa kamati maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Afisa yeyote wa Serikali atakayekwamisha ufanyaji biashara, uwekezaji au uanzishwaji viwanda nchini ni adui namba moja wa Serikali na atachukuliwa hatua za kisheria.

Ametoa wito kwa watendaji hao kuwezesha uwekezaji, ufanyaji biashara, uanzishaji viwanda na kuhakikisha kila mwekezaji anapata anachostahili kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Dkt. Abdallah ameyasema hayo mkoani Kagera alipoongoza Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi inayojumuisha Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara, Fedha, Mipango na Uwekezaji, Kilimo na Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera walipotembelea kiwanda cha sukari cha Kagera kuona hali ya uwekezaji na kutatua changamoto zinazowakabili.

Amesema, Serikali inafuatilia kwa karibu sekta ya uwekezaji na biashara, hivyo yoyote atakayekwamisha jambo lolote kwenye sekta hizo ataondolewa ama kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live