Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ataka CTI kutatua kero za wenye viwanda

77ae4ae617e3a85e5631af6a4ad86619 Ataka CTI kutatua kero za wenye viwanda

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amelitaka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), kuendelea kuwaunganisha wenye viwanda na masoko ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo kushirikiana na mamlaka za serikali kutatua kero za mara kwa mara zinazokwamisha biashara.

Kigahe alisema hayo hivi karibuni alipokutana na CTI ukiwa mkutano wake wa kwanza kukutana na shirikisho hilo.

Alisema katika kutekeleza dhana ya Tanzania ya viwanda, CTI ikiwa kama mwamvuli wa wafanyabiashara, wana jukumu kubwa la kuunganisha masoko na wenye viwanda kwa kuwa ndio wadau wao wa kila siku.

Kigahe alisema kuwa serikali itatekeleza majukumu yake ya kila siku ya kuandaa mazingira mazuri ya biashara, lakini CTI kwa kushirikiana na wenye viwanda wanahitaji kwenda mbele zaidi.

Alisema serikali imeondoa tozo zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara na pia imeziweka pamoja mamlaka zinazohusika moja kwa moja na masuala ya biashara ii watoe huduma kwa ukaribu zaidi.

Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia Utolewaji wa Mizigo (Taffa), Edward Uiro alisema Serikali imefanya jitihada kubwa kuimarisha mazingira ya biashara. Lakini, alisema bado kuna baadhi ya kero zinazotakiwa kufanyiwa kazi.

Alisema wanachama wa chama hicho, wamekuwa wakiwasilisha hoja zinazowakwaza kwenye utoaji wa mizigo na zimekuwa zikitatuliwa moja moja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz