Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asimilia saba mikopo ya biashara inakwenda sekta ya kilimo

Kilimo House Asimilia saba mikopo ya biashara inakwenda sekta ya kilimo

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Mipango na Uwezeshaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kati ya mikopo yote ya kibiashara nchini ambayo ni Sh22 trilioni ni asilimia saba tu ndiyo inayokwenda katika sekta ya kilimo.

Profesa Mkumbo ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 6, 2023 wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa mwaka 2024/25.

Amesema wananchi wengi nchini (asilimia 65.1 ya idadi ya watu wote Tanzania), wanaishi vijijini na kwamba shughuli nyingi za uzalishaji zinategemea kilimo na sekta hiyo imeajiri asilimia 61 ya nguvu kazi.

Pia amesema kasi ya ukuaji wa uchumi vijijini haiendi sambamba na kasi ya ukuaji wa uchumi mijini na ukuaji wa sekta ya uzalishaji viwandani unategemea malighafi kutoka maeneo ya vijijini.

Profesa Mkumbo ambaye ni waziri wa kwanza tangu kuanzishwa kwa wizara hiyo, amesema pia mifumo ya ugharimiaji wa shughuli za kiuchumi haishikamani na shughuli za kilimo vijijini.

“Izingatiwe pia kwamba mifumo ya ugharimiaji wa shughuli za kiuchumi haishikamani na shughuli za kilimo vijijini. Mikopo yote ya kibiashara nchini ni Sh22 trilioni, wakati mikopo inayokwenda katika sekta ya kilimo ni asilimia saba pekee, ” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live