Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 70% za Samaki huharibika kabla ya kufika Sokoni.

Samaki Mulea.jpeg Asilimia 70% za Samaki huharibika kabla ya kufika Sokoni.

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Kati ya asilimia 40 hadi 70 ya samaki wanaovuliwa ziwa Tanganyika uharibika kabla ya kufika sokoni kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwahifadhi hivyo kusababisha hasara kwa wavuvi na Serikali.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi, Dk Ismael Kimirei katika mkutano wa kuthibitisha matokeo ya utafiti wa mnyororo wa thamani wa dagaa na samaki aina ya migebuka uliifanyika mjini Kigoma.

"Kama mvuvi atavua samaki 10 basi wanne kati yao wataoza kabla ya kufika sokoni au kwa sababu wavuvi huku wanategemea jua kukausha, wakati wa mvua madhara hufikia asilimia 70. Ni kwa sababu hakuna mbinu bora za kuwahifadhi kabla ya kuwachakata," amesema Dk Kimerei.

Amesema kwa mwaka ziwa hilo hutoa zaidi ya tani 60,000 za samaki ambao zaidi ya nusu huharibika kabla ya kufika sokoni na hivyo kusababisha hasara kwa wavuvi na serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji, Nazaeli Madala amesema kutokana na hali hiyo Serikali na wadau wameanzisha mradi wa miaka mitano utakaowawezesha wavuvi kupata vifaa bora vya kuvulia na kuhifadhi samaki ili wasiharibike.

Mradi huo wa Fish4ACP unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Wizara ya Uchumi na Maendeleo ya Ujerumani, unatekelezwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika nchi 12 duniani.

Chanzo: Mwananchi