Serikali imesema asali ya Tanzania inayozalishwa Mkoani Tabora imeshika nafasi ya pili kwa ubora kupitia mashindano ya ubora wa asali zinazozalishwa Barani Afrika ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita Tanzania imeuza jumla ya tani elfu 5.6 za asali nje ya Nchi yenye thamani ya USD milioni 40.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (TFS) amesema asali ya Tanzania hupimwa katika maabara za Kimataifa za ithibati kila mwaka na kwa miaka yote Tanzania imepata alama za juu wastani 96/100 “Masoko makubwa yako Nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Uarabuni, Marekani na EAC na SADC”
“Uzalishaji wa mazao ya nyuki Nchini umeongezeka hadi kufikia wastani wa tani elfu 32,691 kutoka tano elfu 31,179 sawa na ongezeko la asilimia 5%”